WAGONJWA 568 wamepata huduma na kutibiwa na Madaktari bingwa walioletwa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan ambao walianza kutoa huduma mei 6,2024 na wamehitimisha zoezi hilo mei 10 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya chacha wambura amesema ujio wa Madaktari hao umepelekea upatikanaji wa fedha kwa mda wa siku tano zaidi ya shilingi Milioni 2 kwa wagonjwa waliopata matibabu bila bima.
Hata hivyo Wambura amemshukuru Rais Samia kwa kuleta Madaktari bingwa ambao wameleta chachu kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma na kwa upande wao Madaktari wamejifunza mambo mengi.
Nae Mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Mussa Rashid amesema kupitia zoezi la Madakri bingwa wamejipanga kuhakikisha wanaboresha utoaji wa huduma za Afya ikiwa Halmashauri hiyo inapokea wagonjwa wengi kutoka Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe.
“niwapongeza sana ujio wenu tumepata faida kwetu sisi na wananchi na wataalam wamejifunza kutoka kwenu kwa mda wa siku tano mmefanya mambo makubwa Mungu awabariki”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Mei10,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa