Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Teofanes Mlelwa amefungua mafunzo ya waganga wa Tiba za asili na Tiba mbadala katika ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na kuhudhuliwa na waganga 23.
Mwenyekiti katika hotuba yake amesema waganga hao wazingatie Miiko na Maadili katika eneo lake la kazi kamavile Mganga awe na heshima wakati wa kutoa huduma,asiwe mbinafsi,aepuke ubaguzi wa dini,utaifa,rangi hali ya kisiasa ,jinsia pamoja na kuepuka uhusiano wa mapenzi na wateja kwa manufaa ya kibinafsi.
Hata hivyo amesema Mganga wa tiba za asili ahakikishe apelike wagonjwa wenye maradhi hatari hospitali,aepuke kutoa siri za wateja,kuwahudumia na kuwatibu wagonjwa kwa maarifa ,ujuzi na mitazamo adilifu,kuepuka kutumia nyumba za wageni kutolea huduma.
“Epuka kumtolea huduma mtoto chini ya miaka 18 bila kuwepo mzazi /mlezi wake,kumtoa mimba kwa kutumia dawa za asili,kutibu kwa kutumia viungo vya binadamu,epuka vitendo vya kichawi lamli chonganishi,ukeketaji pamoja na kukata kimeo”.
Amesema waganga hao wa tiba ya asili na mdabala waepuke kutoa matangazo bila kibali cha baraza mganga huyo atawajibika endapo madhara yatajitokeza kwa mteja pamoja na kumruhusu mtu asiyeidhinishwa kutoa huduma.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasilino Halmashauri ya Madaba
Septemba 26,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa