WADAU mbalimbali wametoa maoni juu ya kutokomeza janga la ukatikili dhidi ya wanawake na watoto Halmashauri ya Wilaya ya Madaba .
Mzee mshauri Winfred Mbilinyi ametoa maoni yake katika kikao cha wadau kuhusu swala nzima la maadili kwa vijana ikiwemo malezi kwa wazazi juu ya watoto wao.
“Watoto wetu miaka hii wamekuwa na sauti zaidi kushinda wazazi,wazazi wanashindwa kuwakemea watoto wao kutokana na hali ya utandawazi”.
Mbilinyi amesema miaka hii vijana wamesahau mira na destuli na kuvamia utandawazi ambao unapelekea mmomonyoko wa maadali.
“Kwa nafasi ya pekee napenda kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona jambo hili la kurudisha machifu na kutambua uwepo wa wazee na kutuanzishia mabaraza ya ushauri”
Amesema swala la maadili ya vijana yanautofauti mkuwa na miaka ya nyuma mtoto akifikia miaka mitatu na kuendelea alikuwa anatumwa na mtu yeyote na kusalimia lilikuwa jambo la lakawaida.
“siku hizi ukisikia mtoto anakusalimia anataka kujua mda au hana nauli au anashida nyigine unakuwa unasalimiwa kwa rushwa maadili mengi yamepungua”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wajasiriamali kijiji cha Ndelenyuma ameiomba serikali kutunga shelia ndogo ambayo itasidia matumizi ya nyumba za wageni pamoja na uvaaji wa wahudumu wao unaopelekea kuvaa mavazi ambayo hayana maadili kwa watoto.
Aidha ametoa rai kwa wazazi kuhakikisha wanaacha kulala na watoto wao mara wanapofikia miaka miwili na kuendelea badala yake wawatengee vyumba vyao.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 25,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa