Mwenge wa Uhuru umezindua miradi nane katika Halmashauri ya Madaba Ukiwemo Mradi wa vyumba viwili vya Mdarasa Shule ya Sekondari Lipupuma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidi Idrisa Mohamed amesema Shule ipo katika Kata ya Mkongotema na ilianzishwa April 23,2007 na kupewa namba ya usajili S3242.
Amesema Mradi wa Vymba viwili vya Madarasa uliibuliwa na wananchi Desemba 2020, kwa kuanza kufyatua tofari na ujenzi wa maboma, ikiwemo ukamilishaji ulianza rasmi Novemba 30,2021 baada ya kupokea fedha za tozo kiasi cha shilingi milioni 25 kutoka Serikali kuu.
Hata hivyo Mkurugenzi amesema lengo la mradi huo ni kuondoa adha ya wanafunzi kubanana katika vyumba vya Madarasa na kusaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika Mitihani ya Kitaifa na kusaidia wanafunzi kusoma katika Mazingira mazuri na kuongeza ari ya kujisomea.
“Mradi umekamilika kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 29 kati ya fedha hizo milioni 25 kutoka Serikali Kuu na milioni 4,860,000 ni nguvu za wananchi zilizojumuisha uchimbaji wa msingi”.
Amesema mradi huo umetekelezwa kupitia utaratibu wa FORCE ACCOUNT ambapo Shule ilinunua vifaa na kuajili fundi wa ujenzi Shughuli za ujenzi ulikuwa chini ya Kamati ya Ujenzi na manunuzi ya Vifaa pamoja na Kamati ya Mapokezi na kukamirisha mradi Machi 01,2021.
“Natoa Shukrani za dhati kwa Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ukamilishaji”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Aprili 15 2022
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa