• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

VIONGOZI wa Dini Ruvuma wamlilia Rais Magufuli

Posted on: March 19th, 2021

Kamati ya Amani Mkoa wa Ruvuma kwa kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na Rais Magufuli wamewaasa wananchi  kuwa watulivu.

Akizungumza katika kikao cha  Kamati ya Amani cha viongozi wa Dini  Mkoa wa RuvumaMwenyekiti  Alhaji Shekhe  Shabani Mbaya  ametoa pole kwa Taifa la Tanzania na kwa mama Janeth Magufuli na familia pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Mzalendo namba moja ametutoka kipenzi cha watanzania tumepatwa na mshituko  mkubwa,tuna majonzi makubwa,kama viongozi wa dini tunamasikitiko makubwa sana ya kuondokewa na Jemedari wa Vita“.

Katibu wa Balaza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) Mchungaji Elimu Mwenzegule  amesema tutamkumbuka kwa mengi ambayo amefanya katika uhai  wake katika kutetea wanyonge na kutopenda mafisadi nchini na wahujumu uchumi.

Mwanzegule amesema Rais Magufuli alipenda nchi ya Tanzania na alihakikisha  inajengwa na watanzania wenyewe katika kipindi chote alicholichokuwa madarakani  alifanya kazi na watanzania hakupenda kutoka nje na alisema ni Rais wa watanzania na aliwatumikia kwa moyo.

“Tumepoteza kiongozi Jemedali na hodari Tunamuombea makamu wa Rais Mungu ampe uvumili  katika kusimamia Maombolezo haya na kumpumzisha Mpendwa wetu, amevipiga vita vilivyo vizuri mwendo ameumaliza,Imani ameilinda  Rais Magufuli katika nchi yetu na mwendo ameumaliza”.

Amesema anawatakia viongozi waendelee kuwa na mshikamano ili kuendeleza kazi nzuri  alizoacha Rais,watanzania tuendelee kuwa pamoja  tushikamane kwa utulivu katika wakati huu mgumu ambao tunapitia kwa tukio hili ambalo hatukulitalajia  tushikamane,tutiane moyo.

Naye Makamu mwenyekiti wa Amani  Mkoa wa Ruvuma  Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Ruvuma Amoal Mwenda kwa upekee wake  na kadri alivyozoeleka kwa kazi nzuri  Mungu alimpa vipawa vyake katika utendaji kazi na kutokuwa na ubaguzi kwa watu wote.

Amesema viongozi wa Dini Mkoa wa Ruvuma tunaungana pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuwaomba wananchi wote kuwa watulivu huku tukishikamana na kuomboleza kwa umoja wetu.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Afisa Habari  Halmashauri ya Madaba

Machi 19,2021.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa