VIONGOZI wa Dini Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamepewa mafunzo ya Malezi , ulinzi na Usalama wa Mtoto.
Mafunzo hayo yametolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya APEC Chuo cha Fursa na Mipango Tanzania Respicius Timanywa yamefanyika katika Shule ya Sekondari Madaba day na kuhudhuliwa na viongozi wa Dini mbalimbali.
Timanywa amesema mafunzo hayo hadi kufikia sasa yametolewa katika Mikoa 15 na Halmashauri zake na kuzungumza na viongozi wa Dini walimu wa malezi,walimu wa Unasihi,walezi wa wanafunzi mashulezi na jamii nyingine inayolea watoto.
“Lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuunga mkono jitihada kubwa ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha malezi ya Mtoto ikiwa ni pamoja na kuzuia ukatili wa kijinsia”.
Hata hivyo Mkurugenzi Timanywa amesema ametoa mafunzo kwa viongozi wa Dini kwasababu ni watu wenyekutoa msaada katika jamii, ni watu wanaoishi na makundi mbalimbali ya watu.
“Viongozi wa Dini Watayafanya mafunzo haya kama mahubiri katika Makanisa yao,Misikiti hatimaye zoezi hili la usalama na malezi ya mtoto litaeleweka kwa wananchi wengi , hatimaye dira ya Serikali na mpango wa Mh. Rais utaimarisha mpango wa watoto na watatimiza ndoto zao”.
Amesema viongozi hao wa Dini wamepokea mafunzo hayo,hivyo kwa kina yatafanyika Septemba 21 hadi 28,2023 kuanzia saa 9 kamili alasiri hadi saa 11 Jioni Shule ya Sekondari Madaba day.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 25,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa