MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Teofanes Mlelwa ametoa rai kwa Waheshimiwa Madiwani kusimamia miradi ya Maendeleo katika Kata zao.
Hayo amesema katika Kikao cha Baraza la Madiwa cha robo ya nne ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkurugenzi na kuwapongeza wataalam kwa kusimamia miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed ametoa rai kwa Waheshimiwa Madiwa kutoa ushirikiano wa kusimamia miradi ya maendeleo inayoletwa na Rais Samia.
“Katika Mwaka huu wa Fedha tunaoanza tunaomba ushirikiano uleule tulioonyesha mwaka wa fedha 2022/2023 tuonyeshe ushirikiano pia katika mwaka mpya wa fedha 2023/2024 pamoja na kuhamasisha wananchi waweze kuipokea miradi ambayo Rais anatulete ”.
Hata hivyo Mkurugenzi amewashukuru wataalam wa Halmashauri hiyo kwa usimamizi wa miradi na kuwaomba kuendelea kushirikiana na waheshimiwa madiwani kwa umoja wa kusimamia miradi hiyo itakayotekelezwa Mwaka mpya wa Fedha 2023/2024.
“Shukrani za pekee zimwendee Mh.Rais Samia kupitia Mbunge wetu Joseph Mhagama akitusemea huko Bungeni pamoja na ninyi waheshimiwa Madiwani”.
Hata hivyo amesema mwaka wa fedha 2022/2023 zimepokelewa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja kwaajili ya ujenzi wa Madarasa na Shule moja mpya .
Mohamed amewaomba Waheshimiwa Madiwani kuisemea miradi hiyo kwa wananchi ili wajue juhudi Rais Samia zinazofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kila wanapofanya mikutano katika Kata zao.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Julai 28,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa