Timu ya wataalam Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoa wa Ruvuma ikiongongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Sajidu Idrisa Mohamed ambaye amemkaimisha Mkuu wa Idara ya Utawala Pendo Chagu wametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Serikali ukiwemo mradi wa Shule mpya ya Sekondari Lilondo,Kituo cha Afya mateteleka,na ujenzi wa vyoo 6 katika shule ya msingi Njegea.
Shule ya Sekondari Lilondo imejengwa kwa shilingi Milioni 560 kupitia mradi wa SEQUIP umekamilika na kuanza kutumika na wanafunzi wa kidato cha kwanza waliojiunga mwezi Januari 2024.
Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Halmashauri ya Madaba inapata fedha kwaajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
Kutoka Kitengo Cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 29,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa