KUFUATIA Wiki ya unjwaji wa Maziwa kitaifa Wataalamu wa Halmshauri ya Wilaya ya Madaba amabyo ni kamati ya Lishe wametoa Elimu ya Unjwaji wa Maziwa katika shule ya Msingi Kifaguro.
Akizungumza katika kampeni ya unjwaji wa Maziwa Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo Neema Bernad amesema wametoa Maziwa Lita 40 kwa wanafunzi hao na kuwaeleza umuhimu wa kunywa Maziwa kwa watoto.
Afisa Lishe amesema watoto wapeleke Elimu ya unywaji wa Maziwa kwa wazazi wahakikishe wanapewa maziwa angalau kwa wiki mara mbili ili kusaidia kuboresha afya ya mtoto.
“Watoto wazuri mkifika nyumbani waambieni wazazi wahakikishe wanawapa maziwa angalau mara mbili kwa siku itawasaidia kuboresha afya zenu”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa