MENEJA wa Shamba la miti Wino Grory Fotunatus akiwakilishwa na muhifadhi wa shamba hilo Matha Ndiyetabula katika maadhimisho ya siku ya wanawake kata ya Gumbiro Halmashauri ya Madaba kwa kutoa mahitaji kwa watu wenye mahitaji maalum yenye thamani ya shilingi laki tatu (300,000/=).
Ndiyetabula amesema mahitaji hayo ni madaftari,taulo za kike,kalamu pamoja na nguo zilizogawiwa kwa watu wa lika zote.
“Sisi watu wa Shamba la Miti Wino tupo mahali hapa tumekuja na vitu vichache tunaomba mvipokee”
Kwa upande wake Diwani wa Viti maalum Vumilia Tawete katika maadhimisho hayo ametoa rai kwa wanawake kuhakikisha wanapinga ukatili wa kijinsia kwa watoto pamoja na kuhakikisha wanawapeleka shule ili kila mtoto apate Elimu.
Hata hivyo Tawete amesema wanawake wafichua watoto wenye ulemavu wanaofichwa ndani badala yake wapelekwe shuleni ikiwa wanahaki ya kupata elimu.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Machi 5,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa