Serikali imetoa miche ya miti 200,000 bure kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kupitia Wakala wa Misitu Wino (TFS) .
Akizungumza mhifadhi mkuu wa Shamba hilo Grory Fotunatus ametoa rai kwa wananchi kutunza misitu ikiwemo miche inayotolewa bure kwa wananchi ili kuepuka uchomaji wa moto hovyo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba inategemea sana mapato yake kupitia kilimo cha miti hivyo ametoa rai kwa wananchi kuchangamkia fursa ya upandaji wa miti ikiwa miche inapatikana bure.
“Nichukue nafasi hii kuwapongeza wananchi wa kata ya Wino maana bila wao hata Halmashauri ingepungukiwa sana kimapato baada ya miaka 10 mbele nasisi tutakuwa juu sana kimapato”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 7,2025.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa