WAKALA wa misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti Wino lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wametoa msaada wa vifaa vya kukamilisha majengo katika taasisi za kidini na Serikali zikiwemo shule za Msingi na Sekondari pamoja na Zahanati zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 39.
Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti wino Grory Fotunatus amekabidhi vifaa hivyo kwa Mbunge wa Jimbo la Madaba Mhe.Joseph Mhagama vikiwemo vifaa vya kanisa la Luthelani ushirika wa Lilondo wametoa nondo rolo 50 na saruji mifuko 100 yenye tahamani ya shilingi milioni 3,325,000/=.
Amesema parokia ya mtakatifu mama wa Mungu Lilondo wametoa mifuko 100 ya saruji sawa na shilingi 1,850,000/=,Kanisa jipya kigango cha matetereka mifuko 200 ya saruji sawa na shilingi Milioni 3,700,000/=,Kanisa la mtakatifu Agustino Madaba mifuko 100 ya saruji sawa na shilingi 1,850,000/=,Sekondari ya Wilma mifuko 200 ya saruji sawa na shilingi milioni 3,700,000/=,zahanati ya Mkongotema mifuko 200 sawa na shilingi milioni 3,700,000/=
Hata hivyo amesema sekondari ya Wino imepata vifaa vya ukarabati wa jengo la utawala thamani yake ni milioni 3,419,000/=,Sekondari ya Madaba mbao,nondo zenye thamani ya shilingi milioni 6,668,000/=,Sekondari ya Mahanje madirisha ya aluminium na vifaa vingine sawa na shilingi milioni 6,216,000/=,Shule ya Msingi Mkwera misumari,nondo,saruji na mabati jumla ya shilingi milioni 5,564,000/=
Mhagama amempongeza muhifadhi Mkuu wa shamba la Miti Wino kwa uhifadhi ambao wanamadaba wananufaika na uhifadhi huo.
“Uhifadhi huu umetunufaisha wanamadaba wote kwa namna moja au nyingine kila kijiji,shule ya msingi,sekondari ambao waliomba msaada TFS wakakosa tunamshukuru muhifadhi mkuu wa Taifa,Mhe.Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa namna ambavyo mmetujali wanamadaba”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 18,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa