MENEJA wa Wakala wa Misitu Shamba la Wino Grory Kassmir amekabidhi mifuko ya Saluji 150 yenye thamani ya shilingi milioni 2,475,000/=kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile.
Zoezi hilo limefanyika katika kijiji cha Ifinga amesema kwaajili ya kuongeza nguvu ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ifinga Halmashauri ya Madaba fedha hizo zimetolewa katika mfuko wa mama Samia kupitia Wakala wa misitu Tanzania.
“Sisi sote ni serikali tukaona tuchangie kijiji cha ifinga tuendelee kuleta chachu ya kuongeza maendeleo ili kuhakikisha Ifinga inaendelea kuwa juu na tutaendelea kushirikiana kwa pamoja tunamsaidia Rais kwa pamoja”.
Hata hivyo Meneja ametoa rai kwa wananchi wa Ifinga kuendelea kutunza misitu na kuhakikishe hakuna moto unaotokea kwenye misitu pamoja na kufuata taratibu za kilimo cha mabonde na milimani.
“Najua sisi tunategemea kilimo cha mabondeni na milimani tuhakikishe tunalima kilimo rafiki tujue kilimo kinaweza kuhatarisha vyanzo vya maji au moto”
Amesema kuna kikosi maalumu ambacho kinaanza kazi kuanzia mwezi wa saba mpaka mwezi wa 12 kikosi cha moto na safari hii kutakuwa na mgambo ambao watapewa ajira ya moja kwa moja kwa wale watakao kidhi vigezo na watalipwa 260,000/=. Kwa mda wa miezi sita.
Mkuu wa Wilaya akipokea Saluji hiyo amewashukuru Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) shamba la Wino ambalo lipo katika Halmashauri ya Madaba
“Tunashukuru sana kwa mifuko ya saluji 150 imetolewa kwaajili ya kuwasaidia wananchi wa Madaba ambao wanaoishi kijiji cha Ifinga na maalumu kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya maana mmewapa heshima wananchi wa kijiji cha hiki asanteni”.
Hata hivyo boma la kituo hicho limejengwa kwa shilingi Milioni 31,000,000/= fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
Kutoa kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 3,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa