WANANCHI wa Halmashauri ya Madaba walioingia katika Mfumo wa TASAF wamenufaika na kuondokana na Umasikini.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri hiyo Juma Komba ametembelea kaya mbalimbali za walengwa wa TASAF na kuangalia maendeleo ya wananchi hao mara baada ya kuingia kwenye mfumo huo kwa zaidi ya miaka mitano na kuona matokeo chanya kwa Juma Nyoni anayepatikana katika Kijiji cha Kipingo Kata ya Lituta.
Afisa maendeleo amejionea kwa walengwa hao kuondokana na hali duni kutoka kuishi katika nyumba ya Nyasi na kujenga Nyumba nzuri ya Kuishi pamoja na kusomesha watoto, kuwa na miradi mbalimbali ya kilimo pamoja na ufugaji.
Mnufaikahuyo Nyoni ameeleza jinsi alivyokuwa anajiwekeza katika vikundi vya kupeana na kununuliana mbolea pamoja na ufugaji wa kuku.
“Toka nimeingia TASAF ni zaidi ya miakamitano nilikuwa na nyumba ya Nyasi nilijiwekeza kwa fedha za TASAF kupitia kikundi na ufugaji”.
Kwa upande wake Helene Hausi Mkazi wa Kijiji cha Ifugwa Kata ya Lituta Halmashauri ya Madaba amesema ameingia kwenye mpango wa TASAF zaidi ya miaka mitano na kumnufaisha katika Nyanja mbalimbali.
Amesema amefanikiwa kwa kutoka kwenye nyumba ya nyasi na kujenga nyumba ya Bati pamoja na kusomesha watoto wake,Kufuga Mbuzi 7 ,kuku 100 pamoja na kilimo , ununuzi wa Tv na kuweka umeme katika nyumba yake.
“TASAF imenisaidia kusomesha watoto,ufugaji wa kuku 100 hadi sasa pamoja na Mbuzi 7 ikiwemo na ujenzi wa Nyumba ya bati na kuepukana na Nyumba ya Nyasi”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Novemba 29,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa