MKUU wa Shule ya Msingi Lipupuma Onesphory Mgina amesoma taarifa ya ujenzi wa Shule kupitia Mradi wa Boost kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas.
Akisoma taarifa hiyo amesma Shule shikizi Lipupuma ilianza rasmi Februari 2023, ikiwa na jumla ya wanafunzi 60 wanafunzi wa awali 30 na darasa la kwanza wanafunzi 30 na walimu 2 mmoja wa kuajiriwa na mmoja wa kujitolea.
Mgina amesema Shule ya Msingi Mkongotema ilipokea fedha ya Ujenzi wa Shule ya Mkondo mmoja shilingi Milioni 331,600,000/= Aprili 24,2023.
Amesema ujenzi huo ni pamoja na madarasa mawili ya mfano ya awali vyoo matundu 6,jengo la utawala na matundu ya vyoo 3,madarasa saba ya Elimu msingi vyoo matundu 8.
Mgina amesema mradi ulitekelezwa kwa mfumo wa njia ya Force account na kusimamia kwa timu mbili za ukaguzi,na timu ya usimamizi na kufikia hatua ya umaliziaji wa vyoo vya wanafunzi na mifumo ya maji pamoja na mitaro ya kupitisha maji katika jengo la Utawala.
“Kiasi cha fedha kilichotumika hadi kufikia sasa Milioni 291,600,000/= na kusalia Milioni 40 kwaajili ya ukamilishaji wa kazi zilizobaki.
Hata hivyo amesema thamani ya nguvu za wananchi ni shilingi Milioni 5,500,000/= kwaajili ya kuchimba Msingi na kujaza kifusi pamoja na kuchimba Mashimo ya vyoo.
Amesma kukamilika kwa mradi huo utasaidia kupunguza umbali wa wanafunzi kuwezesha watoto wengi kuanza darasa la awali,kupunguza msongamano katika shule ya Mkongotema.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba.
Septemba 22,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa