MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed ametoa rai kwa wananchi wa Kata ya Mahanje kuanza ujenzi wa Nyumba ya Mganga kwa nguvu za Wananchi.
Hayo amesema alipozungumza na wananchi hao walipo kabidhi Zahanati kwa wananchi iliyokamilika na kuanza kutoa huduma ikiwa mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri itatenga fedha kwaajili ya umaliziaji wa Nyumba hizo.
“Niwahakikishie tutaitengea bajeti na kuweka vipaumbele vya upatikanaji wa fedha za umaliziaji wa Nyumba hizo pia iweze kupata ruzuku Serikalini”.
Hata hivyo Mkurugenzi amempongeza Meneja wa Tanesco Mkoa wa Ruvuma kwa kuhakikisha analeta Umeme katika Zahanati hiyo.
Diwani wa Kata hiyo Stephano mahundi ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa Zahanati hiyo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama kwa kuhakikisha Zahanati hiyo inakamilika.
Naye Katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Modesta Luoga ametoa rai kwa wananchi wa Mahanje kuhakikisha wanatunza Miundombinu ya Zahanati hiyo ili waweze kujipatia huduma kwa urahisi.
Kwa upande wake katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Juma Nambaila katika zoezi hilo amesema Serikali ya Chama cha Mapinduzi imetoa huduma nyingi kwa Wananchi ikiwemo Afya,elimu, Maji na umeme.
“Kwetu sisi Chama ni Faida kubwa maana tulisimama kwenye majukwaa,tukaahidi na leo tumetekeleza sisi kama chama juhudi zetu ni kusukuma Serikali na wananchi ni wanufanika wa utekelezaji wa Ilani”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Novemba 22,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa