Serikali imesitisha ununuzi wa Mahindi kupitia wakala wa NFRA kwasababu ya changamoto ya ucheleweshwaji wa fedha za malipo kwa wakulima.
Hayo amesema Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile alipoangea na wananchi wa Halmashauri ya Madaba katika uzinduzi wa Ujenzi wa Soko Kata ya Lituta Halmashauri ya Madaba.
“Sisi viongozi wenu tumefanya maarifa tumetafuta wanunuzi wengine wataenda moja kwa moja kwenye AMCOS hatutaki bei za Mahindi zishuke tunataka zipande zaidi”.
Ndile amesema maelekezo ya kusitisha ununuzi wa Mahindi umetolewa na Waziri wa Kilimo Hussen Bashe ikiwa mahindi yaliyopelekwa kwenye vituo vya kunulia yatalipwa .
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 14,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa