Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta fedha kwaajili ya ujenzi wa Mabweni katika shule ya Sekondari Madaba day.
Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama amesema katika ziara yake kuwa shilingi milioni 417 zimeletwa kwaajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya kisasa na madarasa sita pamoja na matundu 10 ya vyoo kupitia mradi wa BARICK.
Mhagama ameambatana na viongozi wa chama cha mapinduzi akiendelea na ziara yake amesema ujenzi wa boma katka shule hiyo umeghalimu kiasi cha shilingi milioni 18 ikiwa milioni sita ilitolewa kupitia mfuko wa jimbo na 12 kutoka kwa wananchi.
“Swala la mabweni katika shule ya sekondari madaba litakuwa limekwisha kwa sehemu kubwa maswala ya kuchangishana yameisha mmebeba mzigo mzito sana”.
Hata hivyo Mhagama amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwa msikivu na kuhakikisha analeta miradi katika Jimbo la Madaba.
“Sekondari hii kwakiasi kikubwa inachukua watoto wetu lakini inachukua na watoto wengine ambao wanatoka maeneo tofauti kidato cha tano na kidato cha sita inawasaidia sana watoto wetu kuwa na uwezo mpana “.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 18,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa