Serikali imeleta fedha kiasi cha shilingi bilioni 1,758,800,000 kwaajili ya ujenzi wa miradi ya Elimu Sekondari na Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Hayo amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed wakati akitoa zawadi kwa shule na walimu waliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2023.
Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta Fedha za uboresha wa miundombinu ya Elimu Sekondari na Msingi.
“Tunamshukuru Rais ametusaidia tumepata fedha nyingi sana zimesaidia kuboresha miundombinu ya Elimu tunavyo vyoo vya kutosha,madarasa na madawati”.
Hata hivyo amesema fedha hizo kwa idara ya elimu sekondari zimeletwa kiasi cha shilingi 1,360,000,000/= na Elimu Msingi imepata shilingi milioni 398,800,000/= kwaajili ya ujenzi wa miundombinu.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 10,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa