• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

SERIKALI Wilaya ya Songea yawaagiza wafanyabiashara kurudisha huduma ndani ya saa 24

Posted on: February 22nd, 2021

SERIKALI wilayani Songea mkoani Ruvuma imewaagiza wafanyabiashara na wasafirishaji abiria waliogoma kurudisha huduma zao ndani ya saa 24 kuanzia saa tisa alasiri Februari 22,2021.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Songea Cosmas Nshenye akizungumza na wanahabari ofisini kwake mjini Songea, amesema kufuatia mgomo unaoendelea amemwagiza Afisa LATRA kufuta mara moja route ya mabasi yote yanayotoa huduma ya usafirishaji kuanzia Songea mjini hadi Mbinga mjini.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa wafanyabiashara wote wenye nia ya kutoa huduma za usafirishaji abiria kutoka Songea mjini hadi Mbinga waombe mara moja kufanya shughuli za usafirishaji katika route hiyo.

Amesema serikali itaendelea kufuatilia mwenendo wa route nyingine za usafirishaji ili kuona ufanisi wake katika kuhudumia wananchi.

“Tuna taarifa kupitia vikao vya wafanyabiashara vilivyofanyika hivi karibuni kuwepo kwa matamshi ya lugha za matusi,uchochezi na uvunjifu wa amani na kuhujumu mipango ya serikali katika kutoa huduma kwa wananchi,hivyo naliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi mara moja na kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wahusika wote watakaobainika kuhusika na vitendo  hivyo’’,alisisitiza Mkuu wa Wilaya.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ameliagiza Jeshi la polisi  na LATRA kuweka mpango mbadala wa haraka wa utatuzi wa suala la usafiri katika kurudisha huduma za usafiri ili kuondoa kero hiyo kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya pia amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea na LATRA kuwachukulia hatua za kisheria kwa mujibu wa Sheria za Leseni ikiwemo kuwanyang’anya leseni za biashara wahusika wote watakaokaidi maelekezo ya kurudi kazini na kufungua biashara zao ndani ya saa 24 kuanzia saa tisa alasiri Februari 22,2021.

Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kusimamia matumizi ya stendi ya Mfaranyaki kama ilivyoamiriwa kupitia vikao vya kisheria vya Baraza la madiwani  la Manispaa ya Songea kwa ajili ya matumizi ya usafiri wa daladala na sio vinginevyo.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Februari 22,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa