MKOA wa Ruvuma wamepewa cheti cha pongezi na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa uzalishaji wa chakula Kitaifa.
Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile alipotembelea eneo la Uwekezaji la Silver Land Ndolela Halmashauri ya Madaba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo .
Hata hivyo Ndile amesema Wawekezaji hao wanapata changamoto ya Barabara kutoka madaba hadi kufika eneo la uwekezaji ni kilomita 30 ambayo kipindi cha Masika magari kukwama njiani na kupelekea vibarua kukwama njiani.
Amesema changamoto za wawekezaji hao ikiwemo Barabara na upatikanaji wa Chokaa kwaajili ya kuchanganya kwenye udongo ,amesema Serikali wamelichukua kwa uzito watalifanyia kazi ili kuhakikisha wawekezaji hao wanafanya kazi zao bila kikwazo.
“Udongo wa Ruvuma hauna shida ya rutuba bali unashida ya tindikali,Kama Mheshimwa Waziri alivyosema analichukua swala hili kwa uzito kutafuta wa wekezaji wa kujenga kiwanda cha kuchakata chokaa”.
Ndile amesema upatikanaji wa kiwanda hicho cha kuchakata Chokaa kitasaidia kupunguza matumizi makubwa ya Mbolea na kitasaidia kuongeza ajira kwa Watanzania na uzalishaji utakuwa wenye tija.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Agosti 24,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa