SERIKALI kupitia Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 5.5 kujenga mradi wa Maji Kata ya Mtiyangimbole Halmashauri ya Madaba.
Mhandisi wa Wilaya ya Songea Mathias Pangras amesema ujenzi wa Mradi huo ulianza Novemba 25,2022 na kukamilika Novemba 25,2023.
Hata hivyo Mhandisi amesema mradi ukikamilika utahudumia Vijiji 3 na wananchi takribani 11,239 mbao watanufaika na mradi huo.
MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile ametembelea na kukagua mradi huo ametoa rai kwa Mkandarasi Names Corporate.Co.Ltd anayejenga mradi huo kuhakikisha anamaliza kwa wakati uliopangwa.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 9,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa