SEKTA ya Elimu Halmashauri ya Madaba mwaka 2021/2022 ilipokea na kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 1 kwaajili ya utekelezaji wa shughuli za Elimu.
Akizungumza Mkuu wa Idara ya Mipango katika kikao cha bajeti cha Baraza la Madiwani amesema Elimu bila malipo ilitengwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 179 zilitolewa kwaajili ya uendeshaji wa Shule za msingi na Shule za Sekondari jumla ya zaidi ya shilingi milioni 206.
Amesema uboreshaji wa miundombinu katika Shule za msingi zilitolewa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 303 kwaajili ya ukamilishaji wa madarasa,matundu ya vyoo na ofisi baadhi ya shule hizo ni Kifaguro,Ngadinda,Likarangiro,Mtyangimbole,Kiblang’ombe,Ngembambili,Mkwela,Mtazamo,Sokoine,Luhimba,Magingo,Njegea,Ifinga,Ifugwa na Igawisenga.
Hata hivyo amesema Shule za Sekondari zililetewa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 718 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 33 vyumba 5 vya maabara,utengenezaji wa viti na meza 1,240 kwa shule 9 za Sekondari.
Afisa mipango amesema Halmashauri hiyo imejenga Shule moja ya Sekondari kupitia mradi wa SEQUIP ambayo ni Shule ya Joseph Kizito Mhagama iliyopo kijiji cha Kipingo Kata ya Lituta.
Luambano amesema hali ya ufaulu elimu ya Msingi ni asilimia 86.1 kwa Darasa la saba na darasa la nne ni asilimia 93.5,Elimu ya sekondari kidato pili asilimia 97,kidato cha nne asilimia 96 na kidato cha sita asilimia 100 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
“Halamshauri hiyo imefanikiwa kupokea walimu 6 msingi 2 na walimu wa Sekondari 4 na wote wameripoti”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Madaba
Februari 7,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa