• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

RUVUMA kuendelea kununua soya na ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani

Posted on: June 26th, 2021

WADAU wa kilimo na Ushirika kutoka wilaya zote mkoani Ruvuma wamekubaliana kuwa hakuna soya wala ufuta utakaonunuliwa  na kutoka nje ya Mkoa wa Ruvuma bila kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Wamepitisha azimio hilo katika mkutano wa uendeshaji wa mfumo wa stakabadhi ghalani uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na kufanyika Ikulu Ndogo mjini Songea.

Mkutano huo umewashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya,makatibu tawala,wakurugenzi wa Halmashauri, wenyeviti wa Halmashauri,Mstahiki Meya,viongozi wa vyama vikuu vya ushirika vya SONAMCU na TAMCU,Mwakilishi kutoka Bodi ya Leseni ya stakabadhi ghalani,maafisa kilimo na watumishi wengine.

“Tumekubaliana wote kwenye kikao hiki,hivyo mkasimamie,hakuna soya wala ufuta utakaonunuliwa kutoka nje ya Mkoa bila kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani’’,amesisitiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

RC Ibuge ameziagiza Halmashauri na wilaya zote mkoani Ruvuma kusimamia kikamilifu utekelezaji huo na kuongeza kuwa Halmashauri zina jukumu la kuunda na kuhuisha  Kamati za usimamizi wa stakabadhi ghalani ili kutatua changamoto ndogo ndogo za wadau.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma pia ameagiza elimu endelevu kuhusu   taratibu,sheria na miongozo iliyopo  katika mfumo wa stakabadhi ghalani ianze kutolewa kila Halmashauri na kwamba vyama vya ushirika vinahusika zaidi ili wadau wapate uelewe wa kina kuhusu umuhimu wa mfumo huo.

Mfumo wa stakabadhi ghalani  katika mazao ya soya na ufuta mkoani Ruvuma,umekuwa msaada katika kuwapatia wakulima kipato kikubwa ambapo takwimu zinaonesha kuwa  msimu wa mwaka 2018/2019 kiasi cha tani 2,855.38 za soya na tani 8,428.27 za ufuta ziliuzwa kupitia mfumo huo na kwamba mwaka 2019/2020 tani 1,499.8 za soya na tani 12,234.76 za ufuta ziliuzwa.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Stephen Ndaki kuwasimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea na Manispaa ya Songea  wanaodaiwa kufanya udanganyifu kuwa sehemu ya ubadhirifu wa kuandika stakabadhi, kuingiza kwenye mfumo wa mapato na kibali.

RC Ibuge amewataja watumishi hao kuwa ni Noel Chengula,Mbaya Kitete na Hamisi Mwanaupanga ambapo Mkuu wa Mkoa  amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma kuwasimamisha kazi ili wapishe taratibu za kisheria.

Mkuu wa Mkoa pia amemwagiza Mkuu wa TAKUKURU kufanya uchunguzi wa haraka ili suala hilo likamilike kisheria,huku akimwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma kufanya ukaguzi katika mfumo wa mapato katika Mkoa na kuwasilisha taarifa kwake Julai 30 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma pia amewaagiza wakuu wa Wilaya  na Kamati za Usalama kufanya kazi ya kufuatilia upotevu wa mapato ya ndani  katika Halmashauri zao na kupeleka taarifa kwake Juni 30 mwaka huu.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewapongeza wafanyabiashara wa mazao mkoani Ruvuma kupitia chama chao cha Umoja wa Wanunuzi wa Mazao Vijijini Mkoa wa Ruvuma (UWAMAVIRU) kuwafichua watumishi wasio kuwa waaminifu na ambao wanatumia vituo vya ukaguzi wa mazao kwa maslahi yao binafsi.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Juni 26,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa