Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kutunza mazingira kwaajili ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.
Thomas amezungumza hayo katika sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi zilizoadhimishwa Kimkoa Manispaa ya Songea viwanja vya Maji Maji.
Hata hivyo amempongeza Mhe .Mkuu wa Wilaya ya Songea kwa kuwakaribisha watumishi na watanzania kutembelea vivutio mbalimbali ambavyo vipo katika Wilaya ya Songea ikiwa bustani ya Ruhila wameletwa Simba 2 na Wanyama wengine mbalimbali.
“Watumishi mpate nafasi ya kutembelea vivutio hivyo kufanya utalii wa ndani na mnapofanya utalii wa ndani mnaondoa stress”.
Mkuu wa Mkoa amesema Kila Mwananchi awe balozi wa kutembelea na kutangaza vivutio vilivyopo katika Mkoa wa Ruvuma na Nchi ya Tanzania.
Hivyo ameagiza kulingana na mabadiliko ya tabia ya Nchi kuhakikisha kila mwananchi anapanda miti ikiwa Mwenge kila ulipopita katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma wamepanda miti.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Halmashauri ya Madaba
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa