• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

RC Ruvuma asikitishwa hali ya malezi na uangalizi wa watoto

Posted on: May 16th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesikitishwa na hali isiyoridhisha ya malezi na uangalizi wa mtoto.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya familia ambayo kimkoa yamefanyika Kijiji cha Suluti wilayani Namtumbo,amesema wazazi na walezi wengi wamekuwa  hawatimizi ipasavyo majukumu ya malezi  na kusababisha malezi ya upande mmoja.

“Takwimu  kutoka ofisi ya Ustawi wa Jamii Mkoa kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2023 zinaonesha kuwa jumla ya mashauri 3,441 yalipokelewa na kushughulikiwa ambapo mashauri 1,611 sawa na asilimia 47 yalihusu matunzo ya watoto,mashauri 831 sawa na asilimia 24 yalihusu matatizo ya ndoa na mashauri 969 sawa na asilimia 29 yalihusu mashauri nje ya ndoa’’,alisema Kanali Abbas.

Amebainisha kuwa Ofisi ya Ustawi wa Jamii imekuwa ikipokea kesi za matunzo ya Watoto na malalamiko yanayoelekezwa upande wa akinababa.

Ametoa rai kwa wazazi na walezi ambao wamefarakana kutambua kuwa mtoto bado anastahili malezi yaliyo bora hivyo ni vema kuweka mpango mzuri wa kumlea mtoto ili asiathirike kimalezi na kwamba wazazi wajitahidi kuvumiliana ili kuepusha kuachana kusiko kwa lazima hivyo kumuathiri mtoto.

Akisoma risala ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya familia Mariam Juma ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ameitaja kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inayosema tukubali tofauti zetu kwenye familia,kuimarisha malezi ya Watoto, inawakumbusha wazazi na walezi kuweka kando tofauti zao na kuangalia malezi na huduma zinazostahili kwenye familia.

Juma amebainisha kuwa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2023 mashauri 2,859 ya ukatili yalitolewa taarifa na kushughulikiwa katika ofisi  za ustawi wa Jamii Mkoa wa Ruvuma na kwamba mashauri 121 yalifikishwa mahakamani.

Hata hivyo amesema mashauri 77  sawa na asilimia 63.6 yalihukumiwa,kati ya mashauri 1,580 ya Watoto,mashauri 1050 sawa na asilimia 66.6 yaliwahusu wasichana wakati mashauri 1,279 ya watu wazima,mashauri 1,030 sawa asilimia 80.5 yaliwahusu wanawake.

Naye Mkuu wa Wilaya ya  Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya amesema wazazi wote wawili wanatakiwa kuwajibika kwa malezi ya familia ili fahari ya mtoto na mafanikio yake yawe kwa wazazi wote wawili kwa kuwa mtoto ni wa wazazi wote.

Amewashauri wazazi na walezi kuwalea Watoto kwa misingi inayompendekeza Mwenyezi Mungu na kuheshimu sheria za nchi,

Hata hivyo Malenya amesisitiza upendo kwa familia ambao unafanikisha malezi bora kwa familia na kutahadharisha kuwa wazazi na walezi wasipoungana kwa dhamira hawataweza kutimiza ndoto za Watoto wao.

Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa Mei 20,1993 lilitenga siku maalum ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya familia lengo likiwa ni kutambua nafasi ya familia katika jamii.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa