Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amelaani vikali wananchi wanaosababisha kukatisha masomo ya wanafunzi kwa kuwapa mimba za utotoni.
Mkuu wa Mkoa amesema hayo alipotembea shule katika Halmashauri ya Madaba siku ya ufunguzi wa shule zilipofunguliwa Kote Nchini Januari 8,2024.
“Watoto wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza,kila mzazi ahakikishe anapeleka mtoto wake na kuhudhuria masomo”.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema faida ya kusomesha wototo hao na kuto katisha masomo yao itawafaidisha wazazi hao hapo baadae na kuona wanafanya kazi katika maeneo mbalimbali wakilitumikia Taifa.
“Tuibebe elimu kwa uchungu mkubwa na nimkombozi juhudi zenu za kujenga shule kwa nguvu zenu ni njema na mama Samia ameamua kuwaleteeni Shule hapa Lilondo ili watoto hao wapate Elimu”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halamashauri ya Wilaya ya Madaba
Januri,8,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa