MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia, Jenerali Wilbert Ibuge amehamasisha kilimo cha Mazao ya Mkakati ili kutatua changamoto ya Uhaba wa Mafuta ya Kula Nchini.
Hayo amesema katika ufunguzi wa mafunzo ya maafisa Ugani 62 katika ngazi ya Mkoa hadi Kata yanayoendelea kwa mda wa siku 3 katika Ukumbi wa Heltage Msamala Manispaa ya Songea.
Ibuge amesema mafunzo haya ya Maafisa ugani yamelenga kuwajengea uwezo katika kuongeza uzalishaji na tija wa zao la Alizeti na mazao mengine ya kimkakati na kipaumbele yakiwemo Soya.
“Niwashukuru washiriki wote kwa kuitika wito na kuja kuhudhuria mafunzo rejea ya kanuni za kilimo bora cha zao la Alizeti,Soya na mazao mengine ili kuongeza uzalishaji na tija pamoja na kuongeza upatikanaji wa malighafi kwaajili ya viwanda,Soko la Ndani na nje ya nchi”.
Hata hivyo amesema Serikali ya awamu ya Sita imedhamiria kuimarisha sekta ya kilimo kwa kubadili kilimo kutoka kuwa cha kujikimu na kuwa cha kisasa chenye tija na chakibiashara.
Amesema matumizi ya teknolojia bora,pembejeo bora,mbegu,mbolea na viuatilifu na kuboresha miundo mbinu katika mnyororo wa thamani ili kuzalisha mazao yatakayokidhi mahitaji ya viwanda vya ndani na ziada kuuzwa nje.
“Wizara imepanga kuboresha huduma za ugani kwa kuwezesha maafisa ugani Kilimo kupata vyombo vya usafiri,mafunzo rejea ya kanuni bora ya kilimo kwa mazao ya Alizeti na Soya pamoja na kuongeza bajeti kutoka milioni 600 2019/2020 hadi kufikia shilingi bilioni 11”.
Mkuu wa Mkoa amesema Serikali imedhamiria katika msimu wa kilimo 2021/2022 kuongeza uzalishaji katika Mikoa yote inayozalisha mazao yenye uhitaji mkubwa katika Soko la ndani na nje ya nchi ili kutekeleza kila afisa ugani kilimo katika ngazi ya Kata na Kijiji awe na Shamba la Mfano shamba darasa ili kutoa fursa kwa wakulima kujifunza kanuni bora za uzalishaji kupitia mashamba.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Ugani na Utafiti kutoaka Wizara ya Kilimo Charles Mjema asemea mafunzo haya yametolewa nchi nzima kwa maafisa ugani 1018 wamenufaika katika kanda mbalimbali.
Mjema amesema kwa Mkoa wa Ruvuma maafi ugani 62 wamefanyiwa mafunzo ili kutatua changamoto ya nchi yetu kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi ikiwemo wataalamu wapo,ardhi nzuri ipo pamoja na hali ya hewa na Kanda mbalimbali zinazoweza kuzalisha mazao hayo.
Afisa Ugani Kata ya Ukili Halmashauri ya Mbinga Mji Hawa Mjiji amesema kupitia mafunzo hayo wataenda kwa wakulima kuhamasisha na kusimamia katika upandaji wa mazao hayo kitaalamu.
Mjiji ameomba ilikufanya kazi vizuri na kupata matokeo mazuri maafisa ugani wanatakiwa kupatiwa vifaa vya kuandaa mashamba darasa pamoja na shamba la mfano ili wakulima waweze kulima kwa tija na kuvuna kwa wingi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Novemba 19,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa