• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

RC IBUGE azindua soko la ununuzi wa mahindi Mkoa wa Ruvuma

Posted on: August 17th, 2021

Mkoa wa Ruvuma una ziada ya mahindi tani 326,497

MKOA wa Ruvuma katika kipindi cha mwaka 2020/2021 umezalisha ziada ya mahindi tani 326,497 kati ya tani za mahindi 816,242 zilizozalishwa.

Akizungumza wakati anazindua soko la ununuzi wa zao la mahindi Kanda ya Songea mkoani Ruvuma katika kijiji cha Mgazini Halmashauri ya Songea,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema katika kipindi cha mwaka 2020/2021,wakulima wa mahindi wameweza kulima jumla ya hekta 276,488.

TAZAMA VIDEO YA UZINDUZI WA SOKO LA MAHINDI HAPA https://www.youtube.com/watch?v=j0jzllfFG0E&t=186s

"Uzalishaji huu ni zaidi ya kiwango kilichozalishwa kwa ongezeko la asilimia nne,ukilinganisha na kiwango cha uzalishaji katika msimu wa mwaka 2019/2020 ambapo tani 787,321 pekee zilizalishwa’’,alisisitiza Ibuge.

Brigedia Jenerali Ibuge amesema Mkoa una uwezo wa kuuza ziada hiyo ya mahindi ndani na nje ya nchi ambapo amewapongeza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA kwa uamuzi wa kununua mahindi ambayo ni sehemu ya ziada.

Amesema katika awamu ya kwanza ya ununuzi kutakuwa na vituo tisa  katika Mkoa wa mzima ambavyo vimepangwa kwa lengo la kumrahisishia mkulima kuweza kununua mahindi yake bila kutumia gharama kubwa.

Hata hivyo amesema kiwango cha kununua tani 32,000 tu za mahindi kwa Mkoa wa Ruvuma ambacho kimewekwa na NFRA ni kidogo ukilinganisha na uzalishaji mkubwa wa mahindi uliofanywa na wakulima msimu huu.

Amesema mgawo huo ni kidogo hivyo ametoa rai kwa Wizara ya Kilimo  kupitia NFRA kuendelea kushirikiana kupanua wigo wa masoko ili wakulima wa Ruvuma waendelee kuzalisha ziada.

Ametoa rai kwa wanunuzi wengine nchini kote  kufika mkoani Ruvuma kuendelea kununua mahindi ili kuipunguza ziada iende kwa wengine nje ya nchi na maeneo mengine yenye uhaba wa chakula ambapo amewaomba kununua kwa bei nzuri ili kuleta tija kwa wakulima na kuwawezesha kulima kwa tija zaidi.

Awali Meneja wa NFRA Kanda ya Songea Ramadhani Nondo  alisema  kwa ujumla NFRA katika msimu wa mwaka 2020/2021,wanatarajia kununua tani za mahindi 165,000 ambapo  Kanda ya Songea imetengewa kununua mahindi tani 32,000 na kwamba kwa awamu ya kwanza zinanunuliwa tani 6,000 za mahindi.

Amesema mahindi yatanunuliwa kwa shilingi 500 kwa kilo katika kituo cha NFRA Ruhuwiko na vituo vingine mahindi yatanunuliwa kwa kilo shilingi 470 na kwamba ununuzi utafanyika kwenye vituo tisa vilivyopangwa ambavyo amevitaja kuwa ni Namtumbo mjini, Namabengo,Mgazini,Magagura,Mpitimbi,Mbinga mjini,Kigonsera na Ofisi za Kanda za NFRA Ruhuwiko.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho ameiomba serikali iongeze kiwango cha tani za ununuzi  kwa sababu wananchi watauza kiasi kidogo cha mahindi ukilinganisha na uzalishaji,hivyo ameshauri  serikali inunue mahindi kupitia mfuko mkuu wa serikali ili yakauzwe kwenye mahitaji ya chakula ndani na nje ya nchi.

Amesisitiza kuwa wananchi wasipotafutiwe masoko ya uhakika ya mazao yao,wataendelea kupata hasara kwa kuuza kwa bei ndogo hali ambayo itawakatisha tamaa kuendelea kulima zao la mahindi.

Mkoa wa Ruvuma kwa mwaka wa tatu mfululizo umeendelea kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwa kuongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Agosti 16,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa