MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jeneral Wilbert Ibuge ametembelea Miradi ya Maji katika Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea.
Ibuge katika ziara hiyo ametembelea chanzo cha Maji cha Igawisenga,Kibandisi na Igombezi na kuwaagiza wataalamu kutoa Elimu naakuwa na makubaliano ya pamoja na wananchi katika swala nzima la kulinda vyanzo vya maji.
Hata hivyo Ibunge amewaagiza viongozi wakiwemo waheshimiwa madiwani kutoa elimu kwa wananchi hao ikiwemo katika swala nzima la kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo ya vyanzo vya Maji.
“Msiseme tumewapa wananchi Elimu wameelewa lazima kuwepo na makubaliano na uelewa wa pamoja ili Maji yawe endelevu ili na vizazi vijavyo waweze kuyakuta”.
Mhandisi Chales Mathias wa Wilaya ya Songea amesema mradi wa Igawisenga ulianza Februali 2021 na kugharimu kiasi cha shilingi milioni 831,229 kwa kuwatumia wataalamu wa ndani.
Mhandisi ameelezea changamoto za ujenzi wa mradi huo ikiwemo kupeleka vifaa kwa kutumia usafiri wa pikipiki wakati wa mvua na mradi haukuweza kukamilika kwa wakati
Mathias ameeleza hali ya utekelezaji wa Maji imefikia asilimia 80 kwa kujenga tanki la Maji la lita laki moja,Nyumba ya Mlinzi, Ununuziwa Mabomba ,ujenzi wa vituo 18 vya kuchotea Maji.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
Octoba 28,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa