RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika tamasha la utamaduni la Kitaifa litakalofanyika Mkoa wa Ruvuma viwanja vya Majimaji kuanzia Septemba 20 hadi 23,2024.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ahmed Abas Ahmed akizungumza katika kikao cha maandalizi ya sherehe hizo ametoa rai kwa viongozi wote kuwa na umoja ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.
“Tumtangulize Mungu katika maandalizi yote ili katika ziara hiyo iweze kufanikiwa”.
Ahmed katika kikao hicho amewapongeza Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi na wataalam wa halmashauri kwa kusimamia miradi,kutatua kero za wananchi na kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato.
Aidha Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wakurugenzi na wasimamizi wa uchaguzi kulipa kipaumbele na umuhimu suala la uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27,2024 kwa kuzingatia miongozo yote ya uchaguzi iliyowekwa.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesisitiza kujihadhari na kujikinga na ugonjwa wa mpox au homa ya nyani ambao umekwisha ingia katika nchi mbalimbali
“Tusijione tuko salama wanapoingia wageni kwenye mipaka yetu tuhakikishe wanapimwa na ugonjwa huo hauna tiba tuchukue tahadhari zote ambazo tumetumia wakati wa ugonjwa wa UVIKO 19”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Septemba 5,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa