MJUMBE wa Umoja wa Wanawake (UWT)Taifa Hawa Ghasia akimwakilisha Marya Chatanda Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania katika Jimbo la Madaba amekagua Mradi wa Maji unaojengwa kwashilingi Bilioni 5.5.
Ghasia amesema katika ziara yake amekuja kukagua miradi yamaendeleo iliyoletwa na Rais Samia kwaajili ya Maendeleo ya wananchi wa Jimbo la Madaba.
Mhandisi wa Wilaya ya Songea Sheila Kimweli akisoma taarifa ya Mradi huo wa Maji unajengwa katika Kijiji cha Mtyangimbole Kata ya Mtyangimbole mradi huo ulianza kujengwa Novemba 25,2022 na kutarajia kukamilika Novemba 25,2023.
Hata hivyo Mhandisi akisoma taarifa amesema mradi ukikamilika utahudumia Vijiji 3 na wananchi takribani 11,239 mbao watanufaika na mradi huo.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Julai,26,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa