KIKAO cha wadau wa maji mkoani Ruvuma kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kimeptisha azimio la kufanya operesheni kabambe ya kuwaondoa wote waliovamia kwenye vyanzo vya maji na kusababisha athari za kimazingira.
Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme anasisitiza kuwa kwa wale ambao wameshalima kwenye vyanzo vya maji na mimea ishaota,msimu huu ni mwisho,
“Tutaendesha operesheni ya kuwaondoa wale wote ambao wanakwenda kulima kwenye vyanzo vya maji na kusababisha watu wengine wapate maji machafu,hili halikubaliki lazima waondoke’’,anasisitiza Mndeme.
Anatoa rai kwa wenyeviti wa Halmashauri zote nane zilizopo katika Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha kuwa suala la kuwaondoa waliovamia vyanzo vya maji linakuwa azimio kwenye vikao vya Baraza la madiwani.
Hata hivyo anasema kwa kuwa hivi sasa waliolima mahindi kwenye vyanzo vya maji,mahindi yamerefuka na tayari wameshaweka mbolea hivyo serikali haiwezi kwenda kung’oa katika msimu huu.
Ametahadharisha kuwa kilimo kwenye vyanzo vya maji kwa kutumia mbolea za kemikali kinaleta madhara makubwa kwa mtumiaji wa maji hayo ambaye anakunywa maji yenye mbolea hali ambayo inaweza kuleta athari za kiafya.
Kutokana na hali hiyo Mndeme amewaomba wadau wote wa maji kutoa elimu ya athari za kuvamia vyanzo vya maji ambapo amesisitiza kuanzia mwakani mtu yeyote ambaye atafanya shughuli za kiuchumi kwenye vyanzo vya maji atachukuliwa hatua kulingana na sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na sheria ya maji ya mwaka 2002 na 2019.
Imeandikwa na Albano Midelo
Februari Mosi,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa