WAJANE Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamepewa elimu ya ufunguzi wa account katika benki ya NMB na kusajili vikundi ili waweze kupatiwa mikopo.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wajane Afisa Mauzo wa benki ya NMB Madaba Jafet Shayo amesema Benki ya NMB inatoa mikopo ya kilimo,ufugaji na biashara mbalimbali.
“Benki ya NMB ili iweze kutoa mikopo lazima kikundi kiwe kinatambulika na Halmashauri na kuwa na account iliyoweka akiba”.
Shayo amesema mkopo wa kilimo riba yake ni asilimia 9 kwa mwaka na kupitia shughuli wanazofanya wanakikundi benki itawakadiria mkopo walioomba.
Aidha ametoa rai kwa wananchi kufungua account rahisi inayoanzia na shilingi 1000 itakayomsaidia mteja kuweka hela sehemu salama.
“Ukitumia account yako ndani ya miezi mitatu itakuwesha kukopa kupitia simu yako mshiko fasta kuanzia shilingi 1,000 hadi 1,000,000/= na kulipa ndani ya mwezi mmoja bila dhamana”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Juni 27,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa