Mbunge wa Jimbo la Malinyi Mkoa wa Morogoro Antipas Ngunguti amempongeza Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama kwa kuwa mshauri mzuri kwa Wabunge wengine.
Ngunguti amesema hayo katika hafla ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Madaba iliyofanyika Kata ya Wino amesema Jimbo la Madaba wamepata Mbunge Jembe ikiwa wanamkakati wa kuhakikisha kijiji cha Ifinga na Malinyi wananchi waweze kufika kwa urahisi na kupata huduma muhimu.
"Mimi na Mhagama tumekaa na kushauriana kwa sababu tumepakana na Kata ya Matumbi na Namtumbo tumepaka na kijiji cha Kitanda".
Aidha amesema wameendelea kuweka mawasiliano baina ya majimbo haya mawili na wameweka mipango ambapo Mbunge wa Madaba ameuanzisha kwa kuungana na Mbunge wa Malinyi kufungua malinyi na Ifinga pawezekufikika.
“Bungeni tunazungumza na kushauriana katika hali ya maeneo yetu ukubalikaji wa Rais katika mambo makubwa anayofanya na ustaarabu, uaminifu wa wapiga kura wa maeneo hayo”.
Hata hivyo Ngunguti amesema Mbunge wa jimbo la Madaba amekuwa akizungumzia maeneo ya Madaba katika kuhakikisha yanapata maendeleo Makubwa na anamapenzi makubwa aliyonayo kwa wanamadaba.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 9,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa