Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Imanuel Nchimbi amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa kumpokea kwa shangwe na ndelemo mara baada ya kuwasili katika Mkoa huo Jimbo la Madaba akitokea Mkoa wa Njombe.
Nchimbi akizungumza na Wananchi ametoa salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano na amempongeza Mbunge wa Jimbo la Madaba kwa niaba ya chama cha mapinduzi kwa kutoa ardhi itumike kwaajili ya Chama cha mapinduzi.
“Kwa uungwana ulionao Mbunge umekabidhi viwanja na majengo yaliyopo tunakushukuru sana”.
Hata hivyo Nchimbi amesema Mbunge wa Jimbo la Madaba kwa kutambua watendaji waliopo kwenye Jimbo lake ametoa pikipiki 8 katika kata kwa makatibu wa chama na baiskeli 45 kwa makatibu wa matawi.
“Nikisema CCM haitamani kuwa na Wabunge wa namna hii nitakuwa muongo inapenda kuwa na wananchama na viongozi ambao wapo tayari kujitoa na kujitolea kwaajili ya chama na Nchi”.
Hata hivyo amesema alichokifanya Joseph Mhagama siku ya leo amenikumbusha historia ya viongozi wakati wa kupigania Uhuru walitoa mali na fedha zao kwaajili ya TANU,ikiwa watu maskini kabisa walichangia shilingi moja ili Mwalimu Nyerere aweze kwenda kupigania uhuru katika umoja wa Mataifa New York.
Nchimbi amesema kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Madaba ni wachapakazi na wakulima wakubwa hivyo atahakikisha chama cha mapinduzi kitaendelea kusimamia Serikali kuwa pembejeo za kilimo zinapatikana kwa wakati.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Aprili 19,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa