NAIBU Waziri wa Maji Maryprica Mahundi amepiga marufuku kufanya shughuri za kilimo katika maeneo ya vyanzo vya Maji.
Hayo amesema jana alipotembelea vyanzo vya Maji katika Kata ya Mateteleka Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma na kukuta wananchi wamefanya uhalibifu wa Misitu inayotunza Maji.
Mara baada ya kukagua vyanzo hivyo na kufuatia malalamiko ya wananchi kupata Maji machafu ametoa tamko la kutofanya shughuli yoyote katika maeneo hayo ambayo yamesababisha vyanzo vingine kukauka.
Mahundi amesema kuwa Maji hayana mbadala kama wananchi watatumia vibaya misitu na kulima maeneo ya vyanzo , ni lengo la Wizara ya Maji kuhakikisha kila mwanchi anapata maji umbari mdogo ili aweze kufanya shughuli zake za kila siku kiurahisi.
“Nimekuja kuwakumbusha wanamateteleka tutunze vyanzo vya Maji,maana Maji hayana Mbadala,utapata mbadala wa kulima lakini siyo Maji”.
Naibu Waziri amesema amesikitishwa na ukataji wa miti ya asili ambayo ilikuwa inasidia kwa kiasi kikubwa kutunza vyanzo vya Maji na kutoa tamko kuacha mara moja kufanya shughuli yoyote katika maeneo hayo.
Hata hivyo Mahundi amesema Wizara ya Maji ipo mbioni kuleta Maji katika Kituo cha afya Mateteleka ambacho Rais Samia ameleta milioni 200 kwaajili ya kuanza ujenzi wa Kituo hicho.
Mbunge wa jimbo la Madaba Joseph Mhagama amewaomba wataalamu wa RUWASA kuwaongezea chanzo cha maji kufuatia kata Mbili kutumia chanzo kimoja imepelekea Maji kutojitosheleza kwa wananchi hao.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
Octoba 13,2021.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa