SHULE ya Msingi Lilondo Kata ya Wino Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wamefanya Mahafari ya 41 ya darasa la Saba Mwaka 2023.
Aliyekuwa Mgeni rasmi katika Mahafari hayo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Teofanes Mlelwa amesema amewapongeza wanafunzi hao kwa uvumilivu wa kukaa Shuleni miaka saba hatimaye kuhitimu Elimu yao ya Msingi.
“Kukaa Shuleni Miaka saba siyo Jambo dogo,kipekee niwapongeze walimu ndio wanaoishi na wanafunzi Miaka saba wanakuja hapa wakiwa wadogo lakini mpaka kufikia miaka saba wanakuwa wanaweza kujitegemea ndiomana wamependeza”.
Mlelwa ametoa rai kwa Wanafunzi hao kuhakikisha wanaendelea na Masomo ya Sekondari hadi Chuo kikuu.
“Mwanafunzi ambaye hata enda Sekondari atakamatwa na kuwekwa ndani pamoja na Mzazi wake natarajia wote 72 wataenda sekondari ‘.
Mwenyekiti amesema wanafunzi hao waliomaliza katika Kata ya Wino wanabahati maana Serikali imeleta shilingi Milioni 490 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya kisasa amabyo Januari 2024 wanafunzi wataanza masomo yao.
“Ndani ya Halmashauri ya Madaba hii ni Shule ya Pili kama ile ya Joseph Mhagama ,nipende kumshukuru kwa dhati ya Moyo wangu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed na Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama kwa kuleta Fedha Kata ya Wino ya ujenzi wa Shule”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halamshauri ya Madaba
Septemba 21,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa