KUFUATIA siku ya wanawake Duniani inayofanyika kila mwaka Machi 8 wanawake Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wametoa masaada wa vitu mbalimbali kwa watu wenye mahitaji maalumu katika Kata ya Ngumbiro.
Akizungumza Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Halmashauri ya Wilaya wa Madaba Birigita Hongo katika maadhimisho hayo amewaasa wanawake kuacha kukopa mikopo ya kausha damu inayopelekea kuyumbisha familia ikiwa mama ni mlezi katika jamiii.
Hongo amesema wanawake wahakikishe wanajiunga katika vikundi ili waweze kupata fursa za kiserikali zinazojitokeza pamoja na kujishughulisha na biashara mbalimbali za kijasiliamari ili kuweza kuleta chachu katika familia.
“Tuamke akina mama tuache kulala anayeongoza Nchi nzima ni mwanamke,lakini kwanini mwanamke ushindwe kuongoza nyumba yako”.
Hongo amesema kaulimbiu ya siku ya Wanawake mwaka 2024 inasema “wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”.
Hata hivyo amesema kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha jamii kuwekeza kwa wanawake ili kuleta usawa wa kijinsia pamoja na kukumbusha umuhimu wa usawa kijinsia katika kuchochea ukuaji wa uchumi,maendeleo jumuishi na ustawi wa jamii kwa maendeleo endelevu kwa wanawake.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Machi 5,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa