Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba ametoa rai kwa wenyeviti wa Vijiji na watendaji wa vijiji kusimamia kamati za mazingira za vijiji ili waweze kupambana na janga la uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbli.
Akizungumza katika zoezi la kugawaji wa vifaa vilivyotolewa na Wakala wa misitu TFS Tanzania katika kijiji cha Mtepa Kata ya Lituta Halmashauri ya Wilaya ya Madaba amesema wahakikishe wanazingatia sheria ndogo ndogo zilizowekwa.
“Naomba sana tuzisimamie zile sheria ili tuweze kuepusha majanga ya moto na tuweze kutunza mazingira”.
Aidha Mwampamba amesema wananchi kufuatia kipindi cha mavuno wahakikihe wanajikatia bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa kwa shilingi elfu 30,000/=kwa watu sita katika familia
“Majanga yanakuja mda wowote uwe na pesa hata usipokuwa na pesa rai yangu kwa sasa tumevuna mazao yetu tutenge elfu 30,000/= ili tuweze kujiunga na bima kwa mwaka mzima magonjwa hayapigi hodi tunaweza kutubiwa katika hospitali zetu”.
Hata hivyo amewataka wazazi kuhakikisha wanajali afya za watoto na kuacha kuhamia mashamabni badala yake wawaandalie lishe bora ili kuepuka udumavu na utapiamlo.
“Tujitaidi sana kuwapa watoto wetu Lishe bora tusijisahau mashambi tukumbuke ndani ya mkoa wetu kuna udumavu na utapiamlo kwa watoto“.
Imeandaliwa na Aneth ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Julai 19,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa