Huduma za Afya za kibingwa zilizotolewa kwa siku tano katika hospitali ya Wilaya ya Madaba wagonjwa 296 wamepatiwa matibabu.
Akizungumza kiongozi wa Madaktari bingwa Phillip Muhochi ambaye ni bingwa wa ganzi na usingizi kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili amesmea katika huduma zilizotolewa kwa wingi katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba ni upande wa Kinywa na Meno ,fizi na majipu kwenye kinywa .
Hata hivyo amesema kwa magonjwa ya ndani madaktari hao wamebaini tatizo la shinikizo la damu,mishipa ya fahamu na maumivu ya mgongo.
Katika suala la upasuaji tumebaini suala la tezi dume kwa asilimia kubwa ngiri au henia na magonjwa ya kina mama tumegundua matatizo ya kukosa ujauzito na mfumo wa upumuaji wa watoto.
“Tumeona na tumeyapatia ufumbuzi matatizo hayo na tumewasaidia watumishi wa afya kwa kuwajengea uwezo namna ya kupata ufumbuzi wa magonjwa na pale inapohitajika rufaa zinazotakiwa”.
Muhochi ameishuru Serikali kupitia mpango huu kwaajili ya kuwasongezea huduma Watanzania wote hata wa vijijini ikiwa kwa hali ya kawaida siyo rahisi kila mwananchi kufuata huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili na mahali kwingine.
“Wito wangu wananchi wanapopata taarifa ya ujio wa madaktari bingwa waje tupo tayari kuwahudumia wananchi na Watanzania wenzetu”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Novemba 1,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa