Muhifadhi wa shamba la miti Wino TFS Grory Fotunatus ametoa rai kwa wananchi wa Madaba kujiunga katika vikundi ili waweze kupewa mizinga ya kufugia nyuki.
Muhifadhi amesema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya ujenzi katika taasisi za kidini na Serikali kwa Mbunge wa Jimbo la Madaba amesema wananchi wahakikishe wanaacha kukata miti na kulima kilimo cha mabondeni badala yake wafuge nyuki.
“Undeni vikundi kupitia halmashauri kuna mizinga 30 pale ofisini vinasubiri kikundi hivyo yote ni jitihada za kuhifadhi mazingira kauli mbiu inasema “achia choka kamata mzinga” tusikate miti ya bondeni inaharibu mazingira”.
Hata hivyo amesema ukataji wa mti mmoja ambao unaweza kuhifadhi mizinga mitano ya nyuki ambapo asali yake inasoko kubwa ndani na nje.
“Kuna fursa ya upandaji miti,mbao wino na igawisenga kuna mzunguko mkubwa wa hela kwasababu walipanda miti na sasahivi wanauza changamkieni fursa ya uhifadhi”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 19,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa