Afisa afya wa halmashauri ya Wilaya ya Madaba Geofrey Mwatwinza ametoa rai kwa wananchi kujikinga na ugonjwa wa Mpox.
Hayo amesema katika kikao cha kamati ya afya ya msingi kufuatia mlipuko wa ugonjwa ambao bado katika nchi ya Tanzania haujaingi.
Mwatwinza amesema kisa cha ugonjwa huo ulibainika kwa mtoto wa umri wa miezi 9 nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) mwaka 1970.
“Awali maambukizi yalianza kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu lakini hata kwa binadamu kwenda kwa binadamu wanaambukizana,Kimataifa mwaka 2022 ugonjwa ulienea katika nchi 100 ambazo hazikuwa na historia ya virusi hivyo”
Amesema dalili za ugonjwa wa Mpox ni homa kali,Maumivu ya kichwa,Maumivu ya Misuli,Maumivu ya mgongo na uchovu wa mwili,kutokwa na vipele vyenye majimaji,hasa maeneo ya usoni,mdomoni,mikononi,miguuni sehemu za siri na sehemu zingine za mwili.
Aidha amesema ugonjwa huo unaambukizwa kupia kugusana,majimaji ya mwili,matapishi,jasho na mkojo,kujamiiana kugusa sehemu zenye vimelea,mjamzito anaweza kuambukiza mtoto aliyepo tumboni.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 28,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa