MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewapongeza wadau wa sekta ya Maji Ruvuma kwa utekelezaji wa miradi ya Maji vijijini na Mijini.
Hayo amesema alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa sekta ya maji katika ukumbi wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma na kuwapa heko wananchi wanaojenga miradi hiyo kwa kujitegemea.
“Ili tuweze kufanya tathimini ya utendaji kazi na uwajibikaji katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maji na kuhakikisha inakuwa endelevu lazima Halmashauri na sekretalieti ya Mkoa muwajibike kikamilifu katika kutekeleza, kusimamia majukumu yote yaliyoorodheshwa kwenye sheria na 5 ya huduma ya maji mwaka 2019”.
Mndeme amesema Meneja wa RUWASA kwa kushirikiana na Halmashauri zihakikishe miradi hiyo na mingine inajengwa na kuunda vyombo huru vya watumia maji na 5 ya mwaka 2019 ifikapo Mei 31, 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amewaagiaza Maafisa Tarafa,Viongozi wote ngazi ya Wilaya na Wakuu wa Wilaya kusimamia utunzaji wa vyanzo vya Maji.
Hata hivyo amesema kikao cha Baraza la Madiwani cha kila robo mwaka iwepo mada ya kudumu ambapo Meneja RUWASA(W) watoe taarifa kuhusu uundaji na usajili wa vyombo vya watumia maji.
Mndeme ameendelea kuwaagiza Mameneja wa RUWASA wa Wilaya kufanya kazi kwa kushirikiana na ofisi za serikali zilizopo kwenye wilaya zao, Halmashauri za serikali za mitaa zote,Ofisi ya Ruwasa Mkoa wa Ruvuma, na Mamlaka ya maji safi wa Mazingira SOUWASA zikishirikiana na ofisi ya Mabonde ya Maji katika kutafuta vyanzo vya maji na kuandaa mpango wa utunzaji wa vyanzo hivyo.
Pia amesema Ofisi za RUWASA Mkoa wa Ruvuma na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira SOUWASA zitumie maabara zilizo kwenye ofisi za mabonde ya maji ili kubainisha ubora wa maji katika kubainisha vyanzo vya maji kwaajili ya miradi.
Amesema Fedha na mauzo ya maji zikaguliwe na wakaguzi wa ndani wa Halmashauri ili kujiridhisha na matumizi ya fedha za wananchi na kuendelea kuchua hatua stahiki kwa wananchi wanao haribu kwa maksudi miundombinu ya maji na vyanzo vya maji.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Februari 1,2021.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa