Kufuatia taarifa zinazosambaa katika mitandao ya Kijamii na kusemekana ni shule ya Msingi Litepetile ambayo ipo katika Halmashauri ya Madaba Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ametembelea eneo hilo leo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed mara baada ya kufika katika eneo hilo amebaini katika Halmashauri hiyo hakuna shule iliyosajiliwa kwa Jina la Litepetile.
“Nimefika katika eneo hili linalosadikika ni Shule ya Msingi Litepetile kutokana na habari iliyosambaa katika mitandao ya kijamii,Halmashauri ya Madaba hatuna Shule iliyosajiliwa kwa jina hilo”.
Mkurugenzi amesema kuna wafugaji wanaohamahama kutafuta marisho ya mifugo yao na wameamua kujitengenezea utaratibu wa kuanzisha Sehemu ya kufundishia watoto wao waliohama nao kutoka sehemu mbalimali.
Hata hivyo Mkurugenzi amesema wengi wao wana mda wa miaka miwili katika eneo hilo na wamesema wanauhitaji wa Shule lakini hawakujua utaratibu wa kufuata na kuanzisha Shule.
”Kama Serikali ya Halmashauri ya Madaba nimeongozana na timu yangu tumetoa maelekezo na utaratibu wa kusajili Shule, nakanusha taarifa iliyosambaa katika mitandao siyo ya kweli badala yake tunashule inaitwa kibula ng’ombe ipo kata ya Mtyangimbole”.
Mkurugenzi ametoa wito kwa wafugaji hao kupeleka watoto wanaoishi katika eneo hilo wakasajiliwe katika Shule ya Msingi Kibulang’ombe ambayo inamamlaka ya kubeba wanafunzi wote na kufuata utaratibu unaotakiwa na siyo kupotosha taarifa na kuleta taharuki katika mitandao ya kijamii.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari mkoa wa Ruvuma
April 22,2022
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa