• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Utawala
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika

MKOA wa Ruvuma watoa chanjo ya polio kwa asilimia 122

Posted on: May 20th, 2022

MKOA wa Ruvuma umefanikiwa kutoa chanjo ya polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa asilimia 122 .

Akizungumza kwenye kikao cha Mkoa cha  utekelezaji wa kampeni ya utoaji wa huduma za chanjo ya polio kilichofanyika mjini Songea,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema Mkoa umepata mafanikio makubwa katika awamu ya kwanza ya utoaji chanjo ya polio.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Pololet Mgema,amesema katika awamu ya kwanza ya utoaji chanjo ya polio,Mkoa ulipanga kuchanja watoto 241,966 ambapo waliochanjwa walikuwa ni watoto 293,543 sawa na asilimia 122.

‘’Mkoa wa Ruvuma umekuwa kinara katika utoaji chanjo ya polio kati ya mikoa minne ya awamu ya kwanza iliyotekeleza kampeni,pia Mkoa wa Ruvuma ulikuwa kinara kwa utaoji chanjo za kawaida mwaka 2021’’.alisisitiza RC Ibuge.

Kwa mujibu wa RC Ibuge, katika chanjo ya UVIKO 19 ambayo Mkoa ulianza kuchanja Agosti 2022,Mkoa umechanja jumla ya watu 409,323 kati yao watu 322,363 sawa na asilimia 78.76 wamekamilisha dozi na watu 86,960 wamepata dozi ya kwanza.

Hata hivyo amesema ili kufikia asilimia 70 ya uchanjaji Mkoa wa Ruvuma,unatakiwa kuchanja watu 670,557 ambao ni asilimia 70 ya watu 957,938 wenye umri wa Zaidi ya miaka 18 ambao ndiyo wenye sifa ya kupatiwa chanjo ya UVIKO.

Amesema hadi kufikia Mei 15 mwaka huu,Mkoa wa Ruvuma umechanja watu 322,363 ambao wamekamilisha dozi sawa na asilimia 48.07 ya watu 670,557.

Kwa upande wake Mratibu wa chanjo Mkoa wa Ruvuma Winbroad Mvile amelitaja lengo la kampeni  za utoaji huduma za chanjo ya polio ya matone kwa watoto chini ya miaka mitano ni kuzuia uwekezekano wa watoto kupata madhara yatokanayo na virusi vya polio.

Hadi sasa visa viwili vya polio vimegundulika katika nchi mbili jirani  na Mkoa wa Ruvuma za Malawi na Msumbiji hivyo chanjo inasaidia kuzuia mlipuko wa ugonjwa huo kwa watoto baada ya kupata chanjo.

Imeandikwa na Albano Midelo

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Mei 19,2022

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA ZA SENSA May 05, 2022
  • TANGAZO LA KAZI May 10, 2021
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • RC Ibuge azisisitiza Halmashauri kutoa Elimu ya Mikopo

    July 01, 2022
  • SERIKALI yatoa bilioni 1.8 kujenga Hospitali Madaba

    July 01, 2022
  • WALIO husika na ubadhirifu mradi wa Hospitali ya Madaba kuchukuliwa hatua

    June 30, 2022
  • HALMASHAURI zote Ruvuma za pata Hati Safi

    June 29, 2022
  • Angalia zote

Video

RC IBUGE AZISISITIZA HALMASHAURI KUTOA ELIMU YA MIKOPO
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 10

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: info@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa