Walimu wa awali Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wanaendelea na mafunzo ya siku nne yanayolenga uboreshaji wa elimu ya awali kupitia mtaala wa elimu uliyoboreshwa wa mwaka 2023.
Akizungumza Mwezeshaji wa Kitaifa kutoka katika chuo cha Ualimu Vikindu Naomi Mjema ikiwa mafunzo hayo yalianza kwa wakufunzi kwa mda wa siku tatu na kuendelea kwa walimu wa awali.
Hata hivyo Mjema ameeleza malengo ya mafunzo ikiwa ni kumjengea mwalimu ujuzi na umahili katika kutumia mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2023 na kumsaidia mwalimu aweze kutumia miongozo mbalimbali ya elimu ya awali.
“Wizara ya Elimu imejalibu kutoa miongozo mbalimbali katika kusaidia kukuza elimu ya awali na kuwa na mafanikio katika mafunzo haya tunatarajia mwalimu ataijua miongozo mbalimbali na ataweza kuitumia kwa ufanisi mtaala na muhuthasari mpya ulioboresha wa mwaka 2023”.
Amesema katika mafunzo haya walimu watajifunza namna ya kufaragua zana ikiwa zana zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu na kujifunza namna ya kutengeneza, mara baada ya mafunzo haya walimu wanatarajia kuwa mahiri sana katika ufundishaji na ujifunzaji katika elimu ya awali na kuwa na dhana za kutosha.
“Tunaamini mafunzo haya yatakuwa na manufaa ya kutosha katika kuwasaidia wanafunzi wa elimu ya awali waweze kukua vyema kiakili,kimwili na maono na katika Nyanja zote za ukuaji”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 18,2025.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa