KUFUATIA agizo la Makamu wa Rais Philip Mpango la Upandaji wa Miti kila Halmashauri ipande miti 1,500,000 Halmashauri ya Madaba inatekeleza kimkakati na kufikia Januari 4,2023 imepanda miti 2000 iliyotolewa na Wakala wa Misitu (TFS).
Hayo yamesemwa na Afisa misitu Halmashauri ya Madaba Erenest Nombo mara baada ya upandaji wa miti 360 katika bonde la mto Nyasa chanzo cha maji cha Mbangamawe Kata ya Ngumbiro.
Kwa Upande wake Mhandisi na Mratibu wa Mazingira RUWASA Sheila Kimweri akiwa na timu yake katika zoezi la upandaji wa miti katika chanzo cha Maji cha Mbangamawe amesema katika Wilaya ya Songea watahakikisha wanapanda miti katika vyanzo vyote vya Maji.
“Tutahakikisha tunapanda miti ambayo ni rafiki katika vyanzo vyote vya maji ambayo hainyonyi maji”.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbangamawe Sallum Abdalah Brash katika zoezi hilo amesema amewapongeza Wakala wa Misitu TFS kwa kutoa miche ya Miti bure ili kuhakikisha vinapandwa katika vyanzo vya maji.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa