Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Teofanes Mlelwa ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanalipa Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa wanawake,vijana na wenye ulemavu.
Hayo amesema katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili ya mwaka 2022/2023 na amewaagiza viongozi wote wa kata kuhakikisha wanasimamia zoezi la marejesho ya mikopo kuwa wote waliokopa wanarejesha ili wengine wakopeshwe na watambue hawakukopeshwa kama zawadi.
“Wote waliokopa warudishe mikopo ili wengine wakopeshwe sababu mkopo huo siyo zawadi“.
Mlelwa amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo pamoja na wataalamu wote kwa usimamiaji wa miradi ya maendeleo.
Hata hivyo mwenyekiti amewaagiza wataalamu kuendelea kukusanya mapato ya ndani ya Halmashauri ili kuhakikisha Halmashauri inakua kiuchumi.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januari 21,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa