WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Angela Kairuki ametoa amaagizo kuhakikisha Walimu wanakuwa na mikakati ya kuboreha ufundishaji kwa wanafunzi Mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dkt Julias Ningu amemwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Angela Kairuki katika kikao Kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Songea girls Manispaa ya Songea na kujumuisha Wakurugenzi wa Halmashauri zote nane,Maafisa Elimu,na walimu wa Kuu wa Shule zote.
Akizungumza katika kikao kazi hicho Ningu amesema kwa niaba ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemiamewataka kuandaa mikakati ya ufundishaji na namna ya kumfanya mwanafunzi aelewe na itasaidia kuleta tija katika Sekta ya Elimu na kuondoa changamoto ya kusababisha dondoko katika Mkoa wa Ruvuma na Nchi nzima .
Amesema kila Afisa Elimu afanye ufuatiliaji mashuleni angalau shule 2 kila siku na kushauriana na walimu kikamilifu juu ya ufundishaji baada ya kukaa ofisini.
Walimu wajiwekee malengo binafsi katika masomo wanayofundisha pamoja na kutambuliwa kwa kazi yao kuhakikisha wanatiwa moyo na kuto dhalilishwi na mtu yoyote.
“ kila kiongozi ahakikishe wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari wanakula Shuleni pamoja na kuhakikisha anaimalisha uwajibikaji wa watumishi wote katika ngazi zote ili kuongeza tija katika utendaji kazi”.
Hata hivyo amesema Walimu wanabahati kubwa sana kwa sababu ni wito ni cheo ambacho hakina kustaafu lakini baada ya kustaafu bado wanaendelea kuitwa walimu inaweza kuwa sababu ya msingi Mwalimu Nyerere katika majina yake alipenda kuitwa Mwalimu.
Naye Naibu Mkurugenzi Tamisemi Suzan Nusu akimwakilisha Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Elimu Mwl. Pauline Nkwama amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa alizindua rasmi miongozo ya usimamizi na utekelezaji wa mikakati ya kuboresha Elimu nchini Agosti 4,2022”.
“Kupitia miongozo ile iligawika Miokoa yote ,Mkoa wa Ruvuma mlifanya vizuri nakili kuhakikisha kuanzia ngazi ya Mkoa Halmashauri mpaka kata”.
Amesema kupitia mikakati hiyo Waziri wa Tamisemi ameelelekeza kukutana na wadau wa Elimu kuelekezana kupewa maagizo kila mtu asimame kwa nafasi yake kuhakikisha jambo watakalokubalina leo lipitishwa na litekelezwa.
Hata hivyo amesema kupitia kikao hiki ngazi ya Wizara wapo kwaajili ya kuweka mikakati na mitazamo ya Serikali pamoja na usimamizi na uendelezaji wa Elimu mwaka 2023 ifikapo Januari 2024 wawe na Lugha moja bila kumtisha mtu bali kufukia malengo ya Wizara ya Rais Tamisemi.
“Mheshimiwa Rais amewekeza sana katika Sekta ya Elimu tufike mahali tuone jitihada za Rais tumekuwa tukifanya vizuri lakini yapo maeneo machache yanatukwamisha hivyo kwa lugha nyingine ya Kikristo kupitia kikao hiki tumebatizwa upya”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Januari 11,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa